TANGAZO MAALUM LA MAFUNZO

TANGAZO MAALUM LA MAFUNZO

September 15, 2025 Online 1 registered
Je, unataka kuliongoza Kanisa au Huduma yako kwa ufanisi zaidi?
Je, unataka kuona maono yako yakibadilika kuwa matokeo halisi yenye tija na athari kwa jamii?
Hii ndiyo nafasi yako!
Mafunzo haya yamebuniwa mahsusi ili kuyapa Makanisa na Huduma zana muhimu za kukua, kustawi, na kuacha alama ya kudumu yenye athari chanya kwa jamii.
SmartLead Consulting Group Tanzania kupitia mradi wake wa Uwezeshaji wa Uongozi Kidijitali inakuletea Mafunzo ya Mipango ya Kimkakati kwa Viongozi wa Kanisa na Huduma.


Kwa Nini Ushiriki Mafunzo Haya?
 Makanisa na Huduma nyingi hukosa mwelekeo wa kimkakati na ulio wazi.
 Viongozi wengi hukutana na changamoto za utawala, uendelevu, na uhamasishaji wa rasilimali.
 Bila mpango ulio rasmi, maono hubaki kuwa ndoto zisizotekelezeka.
Kupitia mafunzo haya utapata:
 Zana za vitendo za kuandaa na kutekeleza mpango wa kimkakati.
 Mwongozo wa kulinganisha maono ya huduma na hatua za utekelezaji.
 Ujuzi wa kuhamasisha rasilimali na kuongoza Timu kwa ufanisi.

Walengwa
 Wachungaji na viongozi wa Makanisa na Huduma
 Wakurugenzi na Waratibu wa huduma mbalimbali
 Viongozi wa huduma za Vijana na Wanawake
Sifa za Mafunzo
 Mfumo mchanganyiko wa ujifunzaji: mtandaoni + warsha za ana kwa ana
 Yataendeshwa na Wakufunzi wabobezi wenye uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya uongozi
 Washiriki wote watapewa Cheti cha Uhitimu kutoka SmartLead Consulting Group Tanzania
Taarifa za Mafunzo
Mafunzo yatafanyika kwa njia ya mtandao (online) kwa muda wa siku 5 mfululizo (Jumatatu – Ijumaa)
• Masaa: Saa 12:00 jioni – 2:00 usiku (masaa 2 kila siku)
• Tarehe za kuanza: Jumatatu, 15 Septemba 2025Gharama: Tsh. 50,000/= kwa kila mshiriki.
Usikose nafasi hii ya kipekee ya kubadilisha maono kuwa matokeo!
Jiandikishe sasa na uwe sehemu ya kizazi kipya cha viongozi wa kanisa na huduma walio tayari kuleta mabadiliko ya kudumu.
Jiandikishe kupitia: www. smartlead.or.tz au kwa barua pepe: info@smartlead.or.tz

Event Information

Date: September 15, 2025

Time: 18:39:00

Location: Online

Price: $80,000.00