Mafunzo ya Mipango ya Kimkakati kwa Viongozi wa Kanisa na Huduma

Mafunzo ya Mipango ya Kimkakati kwa Viongozi wa Kanisa na Huduma

September 21, 2025 Dodoma 1 registered
Mafunzo haya yanalenga kuyapa Makanisa na Huduma zana muhimu za kukua, kustawi, na kuacha alama ya kudumu yenye athari chanya kwa Jamii.
2. Kwa Nini Mafunzo Haya?
• Makanisa na Huduma nyingi hukosa mwelekeo wa kimkakati na ulio wazi.
• Viongozi hukutana na changamoto katika maeneo ya utawala, uendelevu, na uhamasishaji wa rasilimali.
• Bila mpango ulio na muundo rasmi, maono hubaki kuwa ndoto zisizotekelezeka.
Mafunzo yetu yanatoa:
• Zana za vitendo za kuandaa na kutekeleza mipango ya kimkakati.
• Mwongozo wa kulinganisha maono ya huduma na hatua za utekelezaji.
• Ujuzi wa kuhamasisha rasilimali na kuongoza timu kwa ufanisi.
• Msaada wa ujifunzaji kidijitali unaopanua wigo wa kupata mafunzo kwa urahisi.



3. Walengwa
• Wachungaji na viongozi wa Makanisa na Huduma
• Wakurugenzi na waratibu wa huduma mbalimbali
• Viongozi wa huduma za vijana na wanawake
4. Sifa za Mafunzo
• Mfumo mchanganyiko wa mafunzo: mtandaoni pamoja na warsha za ana kwa ana
• Mafunzo yataendeshwa na Wakufunzi waliobobea katika masuala ya uongozi na wenye uzoefu wa muda mrefu.
• Washiriki watapata Cheti cha Uhitimu kutoka SmartLead Consulting Group Tanzania

Event Information

Date: September 21, 2025

Time: To be announced

Location: Dodoma